
Vita haribu na angamizi vya Sudan viinaendelea huku jamii ya kimataifa ikioonekana kushindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro huo wa ndani.
Vita hivyo ni makabiliano kati ya vikosi vya kitaifa vinavyotaka kutetea mamlaka na umoja wa ardhi ya nchi hiyo na wanamgambo wa RFS wanaotishia usalama na uthabiti wa nchi hiyo kupitia vitendo vya ukatili.
Jamii ya kimataifa inakabiliwa na lawama kubwa kutokana na kushinwa kuupatia ufumbuzii mgogoro waa Sudan, huku baadhi ya madola yakilaumiwa kuunga mkono wanamgambo wa RFS.
Mashirika mbalimbali yameendelea kuonya kuhusiana na hali mbaya ya kibinaadamu inayotawala hivi sasa nchini Sudan.
Mapigano ya silaha nchini Sudan yalianza Aprili 15, 2023 kutokana na uchu wa madaraka kati ya majenerali wa kijeshi. Baadhi ya majenerali hao wanaongoza SAF chini ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na kundi la pili ni lile la Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF chini ya Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo maarufu kwa jina la Hemedti.
Vita hivyo vya uchu wa madaraka baina ya majenerali hao wa kijeshi vilizuka baada ya Jenerali Al Burhan kutaka Vikosi vya Msaada wa Haraka viwekwe chini ya jeshi la Sudan kufuati mapinduzi ya 2021 na RSF wakakataa. Hadi sasa kumeshafanyika upatanishi mwingi wa kimataifa lakini umeshindwa kutatua mgogoro wa Sudan.
Katika siku za hivi karibuni na baada ya kutekwa mji wa El Fasher, watawala wa Khartoum, Umoja wa Mataifa na taasisi na mashirika mengine ya kimataifa yamekuwa yakiishutumu RSF kwa kufanya “mauaji ya umati na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya raia wa mji huo.