Mshauri maalumu wa rais wa Marekani kuhusu masuala ya Afrika, Massad Boulos, amekaribisha hatua zilizopigwa na nchi za Rwanda na DRC kuelekea kupata muafaka wa kudumu baina ya pande hizo mbili, baada ya kukutana na viongozi wa nchi hizo mbili.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Boulos ametoa kauli hii baada ya mwishoni mwa juma lililopita kukutana na rais wa DRC, Felix Tschisekedi, ambapo alisema walijadiliana kuhusu namna bora ya kutekeleza makubaliano ya Washington na Doha, ambapo alionesha utayari wa nchi yake.

Aidha kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, Boulos, alithibitisha pia kukutana na Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Olivier Nduhungirehe, ambapo walijadiliana kuhusu hatua zilizopigwa na pande hizo hadi sasa kuelekea kupata mkataba wa amani.

Boulos, amesisitiza umuhimu wa kutekeleza kikamilifu na haraka mkataba wa amani wa Washington, huku akionesha kuridhishwa na utayari wa Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kufikia lengo la mazungumzo yanayoendelea.

Mazungumzo haya yamefanyika wakati huu kukiripotiwa ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M23.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *