Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumamosi, Novemba 1, alisema kwamba anaandaa uwezekano wa kuingilia kijeshi nchini Nigeria ikiwa Abuja haitakomesha kile alichokiita “kampeni ya mateso” dhidi ya Wakristo, ambayo anaihusisha na makundi ya wanajihadi. Abuja inakanusha shutuma hizi, pamoja na tafsiri yoyote ya kidini pekee ya vurugu zinazoendelea nchini humo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe uliotumwa kwenye mitandao ya kijamii, Rais Bola Tinubu amekanusha kwamba Wakristo walikuwa wakilengwa zaidi ya jamii zingine. Siku ya Jumapili, Novemba 2, mmoja wa washauri wake wa mawasiliano amependekeza kwamba wakuu hao wawili wa nchi wanajadili jambo hilo moja kwa moja.

Operesheni “ya haraka na kali”. Hilo ndilo Donald Trump analoahidi katika machapisho yake, akiishutumu mamlaka ya Nigeria kwa kukaa kimya licha ya “uwepo wa tishio,” anasema, ambalo linawakabili Wakristo nchini Nigeria.

Shutuma hizi zinajirudia mara kwa mara kwa wanasiasa wa kihafidhina wa Marekani, hasa miongoni mwa wanasiasa wa kiinjili. Mnamo mwezi Machi, wajumbe wa Bunge la Marekani waliongoza kampeni katika Bunge la Seneti wakitaka vikwazo dhidi ya Abuja. Kila wakati, watafiti na wachambuzi wanasisitiza kwamba shutuma zao hazitegemei ushahidi wowote wa kisayansi.

“Donald Trump ana mtindo wake wa mawasiliano.” Huko Abuja, wamejibu, lakini hali hiyo inapuuzwa. Nigeria “haichukulii ujumbe wa Trump kihalisi,” ameeleza afisa wa mawasiliano katika ikulu ya rais siku ya Jumapili, Novemba 2, akibainisha kuwa “Donald Trump ana mtindo wake wa mawasiliano.”

Msemaji huyo, kidiplomasia, almesema “amekaribisha msaada wa Marekani katika mapambano dhidi ya ugaidi,” mradi, ameongeza, “kwamba uadilifu wetu wa eneo unaheshimiwa.” Hatimaye amependekeza mkutano wa pande mbili, akibaini kwamba “viongozi wanapokutana, matokeo huwa bora zaidi.”

Washington haikubainisha Jumapili jioni kama majadiliano yalikuwa tayari yanaendelea kuhusu jambo hili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *