Saa chache baada ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani, kuiweka Nigeria katika orodha ya nchi zilizo chini ya uangalizi kutokana na mauaji ya Wakristo, utawala wa Abuja umetupilia mbali madai ya rais Donald Trump kuwa wakristo kwenye nchi hiyo wanakabiliwa na tishio la kutoweka.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, rais wa Nigeria, Bola Tinubu, alieleza kuwa katiba ya nchi hiyo inawalinda raia wa imani zote, huku pia akionesha nia ya kushirikiana na Washington kutoa hakikisho zaidi la usalama kwa raia wake.

Siku ya Jumamosi, rais Trump kupitia ukurasa wake wa mtandao wa True Social, alitoa madai kuwa wakristo wamekuwa wakiuawa nchini Nigeria, akiwanyooshea kidole cha lawama makundi aliyoyaita ya wasilamu wenye itikadi Kali ambapo akatangaza kuiweka nchi hiyo ‘chini ya uangalizi’.

Kufuatia kauli ya rais Tinubu, wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo ilitoa tarifa nyingine ya kina kukanusha serikali kutotoa ulinzi kwa Waislamu, ikiyataja madai ya Trump kwa sio ya kweli na kwamba licha ya ongezeko la mashambulio dhidi ya Wakristo, waislamu pia wamekuwa wakilengwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *