Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameapishwa siku ya Jumatatu kwa muhula wake wa kwanza wa kuchaguliwa baada ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi uliozua maandamano makubwa kote chini.

Alikula kiapo katika sherehe rasmi za kijeshi kwenye mji mkuu wa Dodoma.

Samia, ambaye aliingia madarakani mwaka 2021 kufuatia kifo cha mtangulizi wake, alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa wiki iliyopita kwa asilimia 97.66 ya kura.

Samia mwenye umri wa miaka 65, alikabiliana na wagombea kutoka vyama vidogo baada ya wapinzani wake wakuu kutoka vyama viwili vikuu vya upinzani kuondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *