Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameapishwa leo Jumatatu kuiongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano chini ya ulinzi mkali. Anaapishwa baada ya uchaguzi uliokumbwa na maandamano yenye ghasia.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais Samia Suluhu Hassan amekula kiapo chake mbele ya Jaji Mkuu Ibrahim Hamis Juma, akiahidi “kulinda na kutetea Katiba na umoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Naye Emmanuel Nchimbi pia ameapishwa kuwa Makamu wa Rais.

“Mimi, Samia Suluhu Hassan, naapa kwamba nitatimiza majukumu yangu kama Rais wa Jamhuri […] kwa bidii na moyo wa dhati,” amesema mkuu wa nchi, ambaye alivaa kitambaa chekundu kichwani na gauni refu jeusi.

Katika hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa, Rais Samia Suluhu Hassan amewashukuru wanasiasa walioshiriki uchaguzi ikiwemo wagombea wengine 16 waliowania kiti cha urais.

Amesema, yeye na “wote tunaoitakia mema nchi hii, tumesikitishwa na kuhuzunishwa na matukio ya uvunjifu wa amani, upotevu wa maisha na uharibifu wa mali…hasa kwenye majiji na miji”. 

“kilichotokea hakiendani na sifa na taswira ya Kitanzania” na kwamba siyo “Utanzania”. Kiongozi huyo pia amedai kuwa baadhi ya vijana waliokamatwa kwenye wimbi hilo la maandamano ya umma walitoka nje ya Tanzania.

Viongozi kadhaa wa Afrika wanahudhuria sherehe za kuapishwa Samia Suluhu Hassan. Miongoni mwao ni Rais Daniel Chapo wa Msumbiji, Hakainde Hichilema wa Zambia na Evariste Ndayishimiye wa Burundi

Wengine ni Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, Naibu Rais wa Kenya Kithure Kindiki na wawakilishi wa Uganda, Zimbabwe na visiwa vya Comoro. Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ambaye aliapishwa Jumamosi iliyopita baada ya kushinda uchaguzi naye anahudhuria sherehe hizo.

Samia Suluhu Hassan lipandishwa cheo hadi kuwa rais wa Tanzania kufuatia kifo cha John Magufuli mwaka wa 2021 na anatuhumiwa kuendesha ukandamizaji mkali, baada ya hapo awali kulegeza vikwazo vilivyowekwa na mtangulizi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *