Tehran na eneo linaloizunguka ziko hatarini kukosa maji ya kunywa ndani ya wiki mbili kutokana na ukame usio wa kawaida. Mabwawa kadhaa yamekauka na imekuwa vigumu kusambaza maji katika mji mkuu, na bwawa kuu lina maji ya wiki mbili tu yaliyosalia.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na afisa wa serikali, bwawa kuu linalotoa maji ya kunywa katika mji mkuu lina wiki mbili tu zinazosalia maji yakauke kabisa, anaripoti mwandishi wetu huko Tehran, Siavosh Ghazi.

Bwawa la Amir Kabir, moja kati ya matano yanayosambaza maji ya kunywa Tehran, “lina maji ya ujazo milioni 14 pekee, au milioni 8 ya uwezo wake,” kulingana na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya maji ya mji mkuu, Behzad Parsa, ambaye alilinukuliwa siku ya Jumapili, Novemba 2, na shirika la habari la IRNA. Mwaka mmoja uliopita wakati huu, bwawa hilo lilikuwa na maji ya takriban mita za ujazo milioni 86, afisa huyo aliongeza, akihusisha kushuka huko kwa kasi na “kupungua kwa mvua kwa 100%” huko Tehran na eneo linaloizunguka.

“Uhaba halisi”

Hili linaweza kuwa na atharikubwa kwa Tehran na miji inayoizunguka, hasa Karaj, ambayo kwa pamoja ina idadi ya watu zaidi ya milioni 20.

Kuna wasiwasi mkubwa, anasema Babak, mtunza bustani anayefanya kazi Tehran: “Mvua haijanyesha kwa miaka sita. Kuna uhaba halisi. Wakati wa kiangazi, katika baadhi ya vitongoji maarufu kusini mwa Tehran, kulikuwa na maji kwenye mabomba kwa saa mbili tu kwa siku, na nguvu ya maji ilikuwa ya chini sana kiasi kwamba huwezi hata kuoga. Na halii hii inaanza tena sasa. Kutokana na tulichosikia, hakuna maji katika bwawa la Karaj.”

Ukame, ambao umedumu kwa miaka sita, unaathiri nchi nzima, haswa miji ya Isfahan, Hamadan, na Mashhad. Serikali imewaomba raia kupunguza matumizi yao ya maji kwa 25% kwa kila mtu.

Ukame huo hauathiri tu wakazi wa miji mikubwa bali pia kilimo. Uzalishaji wa ngano umepungua kwa zaidi ya 30% kutokana na ukosefu wa mvua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *