Tangu Oktoba 26, mji wa El-Fasher umeangukia mikononi mwa wanamgambo wa RSF wa Jenerali Hemedti. Umoja wa Mataifa unazungumzia “vitendo vya kkatili,” na mashirika kadhaa ya kibinadamu yanaripoti uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanywa dhidi ya raia. 

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko N’Djamena, Nadia Ben Mahfoudh

Angalau watu 2,000 wameuawa na zaidi ya 70,000 wamekimbia makazi yao katika wiki moja tu. Katika nchi jirani ya Chad, ambayo tayari inawapa hifadhi wakimbizi karibu milioni 1.5 wa Sudan, kuna uwezekano ikapokea wakimbizi zaidi kutoak mji huo wa Sudan.

Raia wanaokimbia El-Fasher tangu kuanguka kwake bado hawajafika Chad, lakini kutokana na mwisho wa msimu wa mvua, mamlaka ya Chad na UNHCR wanatarajia kupokea zaidi ya wakimbizi 120,000 kutoka Sudan. Ikiwa kaskazini mashariki mwa Chad, si mbali na mpaka wa Sudan, miji ya Tiné na Kariari ndiyo sehemu mbili kuu wakimbizi wa Sudan wanaokimbia mzozo huko El-Fasher wanatazalia kuwasili.

Mratibu mkuu wa hali ya UNHCR mashariki mwa Chad, Patrice Ahouansou, anasema kwamba karibu Wasudan 100,000 wamewasili kupitia miji hii miwili tangu mwezi Aprili. Njia inayowaunganisha na El-Fasher inachukuliwa kuwa fupi zaidi, lakini pia ni hatari zaidi na ghali zaidi. Vituo kadhaa vya ukaguzi vinavyolindwa na RSF vimewekwa hapo. Ushuhuda wa wakimbizi unaripoti vitendo vingi vya ukatili, ikiwa ni pamoja na ukatili wa kijinsia.

Tukitoroka El-Fasher na kuwasili Garni baada ya kutembea kwa saa 10, tulikutana na wanajeshi wa RSF. Walitusimamisha na kutupora. Walitupekua kwa uangalifu, wakichukua kila kitu tulichokuwa nacho. Hata walipekua sehemu za siri za wanawake.

Hawa, mwanamke mjamzito wa miezi minane, alikimbia na watoto wake, ambao wana umri wa kati ya miaka 2 na 12, amesema Houda Ibrahim.

Wasudan 90,000 wanatarajiwa nchini Chad ifikapo mwisho wa mwaka

UNHCR, kwa kushirikiana na mamlaka ya Chad, imetekeleza mpango wa kuwahamisha wakimbizi kutoka sehemu za kuwasili hadi kambi zilizo mbali zaidi na mpaka.

Chanzo cha Chad mashariki mwa nchi kinasema kwamba “ni kipaumbele kupunguza msongamano katika miji ya mpakani (…) lengo likiwa ni kuepuka janga kubwa zaidi la kibinadamu iwapo mzozo utaenea katika ardhi ya Chad.” Chanzo cha serikali kinathibitisha shughuli kali za ndege zisizo na rubani katika eneo la Sudan kilomita chache kutoka TinĂ©. UNHCR na mamlaka ya Chad wanasisitiza kwamba mpaka wa Sudan na Chad unabaki wazi na kwamba hakuna vivuko vya raia vinavyozuiwa.

Watu wanahama usiku tu. Hawasafiri kwa gari bali kwa miguu, kwa mikokoteni. Wanahama kwa idadi ndogo. Kwa kawaida huchukua angalau siku 10 kwetu kupata dalili yoyote ya kuingia kwa watu kwa mara ya kwanza.

Kutokana na umbali na viziwizi vilivyowekwa na RSF, wa kundi la kwanza lingeweza kufika mapema mwishoni mwa wiki, kulingana na Antony Akumu Abogi, Naibu Mwakilishi wa UNHCR nchini Chad.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *