
Kiongozi wa kijeshi nchini Guinea, Mamady Doumbouya, ameingia rasmi katika kinyanganyiro cha urais baada ya hapo jana kuwasilisha rasmi karatasi za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea katika uchaguzi wa Disemba 28, uchaguzi unaolenga kurejesha utawala wa kikatiba kufuatia mapinduzi yam waka 2021.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua ya Doumbouya, inathibitisha rasmi hofu waliyokuwa nayo wanasiasa wa upinzani Pamoja na wanaharakati kuhusu kile walichodai kuwa njama za wanajeshi kutaka kubaki madarakani hata baada ya uchaguzi mkuu unaolenga kurejesha utawala wa kiraia.
Vyombo vya Habari nchini humo viliripoti kiongozi huyo kuwasili katika mahakama ya juu akiwa chini ya ulinzi wa vikosi maalumu, ambapo baada ya kukabidhi fimu hizo aliondoka bila kuzungumza na wanahabari.
Mwezi Septemba mwaka huu raia wa Guinea walipiga kura kupitisha mabadiliko ya katiba ambayo yaliyopelekea kuitishwa kwa uchaguzi Pamoja na kumruhuru Doumbouya kugombea katika uchaguzi ujao.
Licha ya kutoa ahadi kurejesha utawala wa kiraia na kuruhusu uhuru wa maoni, jenerali Doumbouya na serikali yake wamekuwa vinara kiminya uhuru wa vyombo vya Habari na maoni, ambapo baadhi ya wanahabari wanazuiliwa na vyombo kadhaa vya Habari kufungiwa.