Wizara ya Afya ya Serikali ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umetega mabomu kwenye wanasesere ili kuwaua watoto wa Palestina.

Munir Al-Barsh, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza, ametangaza kwamba jeshi la utawala vamizi wa Israel linatumia wanasesere  waliotegwa mabomu kuwarubuni watoto na limeacha vinyago na wanasesere hao katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza. Amesema, watoto wanalipukiwa na wanasesere na vinyago hivyo wanapovigusa kwa ajili ya kucheza.

Tangu kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano mnamo Oktoba 11, 2025, Wapalestina 238 wameuawa na wengine 600 wamejeruhiwa.

Katika kipindi hicho, miili ya mashahidi 510 pia imepatikana kutoka kwenye vifusi vya nyumba zilizoharibiwa kwa mabomu na ndege za kivita za utawala haramu wa Isarel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *