Merz ameyasema hayo wakati viongozi wa chama chake cha kihafidhina wakilenga kuepusha ongezeko la wafuasi wa mrengo wa kulia kabla ya msururu wa uchaguzi wa majimbo mwaka ujao.

Ujerumani ilikuwa nchi ya Umoja wa Ulaya iliyopokea idadi kubwa zaidi ya wakimbizikutoka vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria vya miaka 14, kutokana na sera ya wazi ya Kansela wa zamani Angela Merkel. Mpaka sasa kuna Wasyria wapatao milioni moja wanaoishi nchini humo.

Lakini Merz na wahafidhina wenzake kadhaa katika baraza lake la mawaziri la serikali ya muungano wanasema hali imebadilika kufuatia kuanguka kwa serikali ya Bashar al-Assad Desemba mwaka jana na kumalizika kwa vita. Hiyo ni licha ya ukweli kwamba Syria bado iko katika mgogoro mkubwa wa kibinadamu na kurejea kwa nguvu kutakabiliwa na changamoto kubwa za kisheria. Merz amesema wataanza mchakato wa kuwarejesha makwao akiongeza kuwa anatarajia Wasyria wengi kurudi kwa hiari ili kuijenga nchi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *