
Ikiwa kesi yake imesikilizwa tangu mwezi Novemba 2024 kwa kutumia vibaya mamlaka yake kwa kujikusanyia utajiri mkubwa, Mahakama Kuu ya Mauritania imetuplia mbali rufaa ya rais wa zamani Mohamed Ould Abdel Aziz siku ya Jumanne, Novemba 4, 2025.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mohamed Ould Abdel Aziz, ambaye awali alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela, alipokea kifungo cha miaka 15 mwezi Mei 2025, badala ya miaka mitano ya awali, kwa “utajiri haramu” na “ushawishi wa biashara.”
Utajiri wa Mohamed Ould Abdel Aziz unakadiriwa kuwa euro milioni 67. Kulingana na mwendesha mashtaka, nafasi ya mkuu wa zamani wa nchi ilimuwezesha, wakati huo, kutumia nafasi yake kuweka shinikizo kwa wawekezaji.
Akiwa na umri wa miaka 69, na baada ya zaidi ya miaka kumi akiwa mkuu wa Mauritania (kuanzia mwaka 2008 hadi 2019), Mohamed Ould Abdel Aziz anakuwa mmoja wa wakuu wachache wa zamani wa nchi hii waliohukumiwa kwa utajiri haramu akiwa madarakani.
Akiwa kizuizini tangu Januari 24, 2023 baada ya kukaa kizuizini kwa miezi kadhaa mwaka 2021, Mohamed Ould Abdel Aziz anaendelea kukumbwa na hali nzito chini ya utawala wa mrithi wake, Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani, ambaye hata hivyo alikuwa mmoja wa vibaraka wake waaminifu zaidi hapo awali.