Waraka wa siri wa jeshi la Israel umefichua kwamba mtu aliyeshambuliwa kikatili na kubakwa na kundi la wanajeshi wa Israel katika gereza maarufu la Sde Teiman mnamo Julai mwaka jana hajawahi kushtakiwa kwa uhalifu wowote na alikuwa raia, kinyume na madai kwamba alikuwa na mwanachama harakati za mapambano ya Hamas.

Kwa miezi kadhaa, watetezi wa utawala wa Tel Aviv wamekuwa wakidai kwamba Mpalestina huyo alikuwa mwanachama wa ngazi za juu wa kitengo cha Nukhba cha Hamas, na kwamba alishiriki katika operesheni kubwa na ya kushtukiza dhidi ya Israel, iliyopewa jina la Operesheni Kimbunga cha al-Aqsa, Oktoba 7, 2023, ili kuhalalisha ukatili huo.

Hata hivyo waraka uliovuja unathibitisha kwamba alikuwa mmoja kati ya raia 1,700 Wapalestina wa Gaza waliokamatwa bila mashtaka na kuachiliwa kutoka kwenye vizuizi vya Israel wakati wa ubadilishanaji wa hivi karibuni wa mateka baina ya Israel na Hamas.

Israel inaendelea kuwashikilia Wapalestina zaidi ya 9,000, na zaidi ya nusu yao wanawekwa kizuizini bila mashtaka rasmi.

Mkanda wa video wa ubakaji huo ulivujishwa kwenye vyombo vya habari mwanzoni mwa Agosti 2024 kufuatia kukamatwa kwa wanajeshi kadhaa wa Israel kwa tuhuma za kumbaka mfungwa wa Kipalestina.

Katika mkanda huo uliovuja, wanajeshi wa Israel wanaonekana wakimkamata na kumpeleka mfungwa Mpalestina aliyekuwa amefungwa macho kabla ya kumzunguka kwa ngao ili kuficha ubakaji huo.

Wakati huo huo, wanajeshi wa Israel waliopatikana na hatia ya kumtesa na kumbaka mfungwa huyo Mpalestina katika kituo maarufu cha Sde Teiman wametetea waziwazi matendo yao, wakisisitiza kwamba wanastahili shukrani kwa walichokifanya.

Wanajeshi hao, waliokuwa wamevaa barakoa nyeusi kuficha utambulisho wao, walitoa matamshi yao wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika nje ya kile kinachoitwa Mahakama Kuu huko Quds Magharibi siku ya Jumatatu.

Wanajeshi wabakaji wa Israel

“Nimesimama hapa leo kwa sababu nimechoshwa na ukimya. Badala ya shukrani (kwa tuliyomfanyia mfungwa Mpalestina) , tumefunguliwa mashtaka,” Channel 7 ya Israel imemnukuu mmoja wa wanajeshi walioshtakiwa, ambaye alitambulishwa kwa herufi ya “A”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *