
Miezi 10 baada ya waasi wa M23/AFC kuudhibiti Mji wa Goma, Mashariki mwa DRC, wakaazi wa bado wanakumbwa na changamoto ya kupata huduma za kifedha, baada ya benki na vituo vingine vinavyotoa huduma hiyo kufungwa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wananchi hao wanadai kwamba hali hii inawatia hofu na kuathiri shughuli zao za kiuchumi.
“Ni kweli kufungwa kwa benki kumetuongezea mateso kwa sababu pesa zimo ndani ya Benki lakini tatizo kubwa nikuzifikia.”
Baadhi ya familia katika mji wa huu wa Goma, zinadai kuishi katika mazingira magumu, hasa wakati huu ambamo milango ya Benki imeendelea kufungwa kwa zaidi ya miezi 9 sasa .
“kwa sasa maisha yamekuwa mazito sana sababu kila kitu kimebaki humo natunashindwa jinsi yakufanya kazi hata pesa zakuliapa shule ni shida “.
Hali hii inaonekana kuathiri si tu maisha ya kila siku ya wananchi bali pia maendeleo ya kiuchumi ya eneo hili. Deo machozi Bengeya ni mtaalamu wa uchumi mashariki mwa kongo.
“Hakuna namna yakufanya kazi vizuri iwapo mtu anapata mshahara kutoka nje ya nchi ya DRC inakuwa ni nguvu sana “.
Haya yanajiri wakati dola za marekani zikishuka thamani mbele ya faranga za kongo,ambapo sarafu ya kongo sasa inaonyesha kushuka kidogo, na kiwango cha mauzo kufikia elfu mbili miatatu na amsini faranga za kongo kwa dola moja ya marekani . Hata hivyo imekuwa ni vigumu kwa wananchi waishio kwenye maeneo yanayokaliwa na AFC/M23 kufikia pesa zao kufuatia kukwama huko kwa huduma za benki.