
Hayo ni wakati huduma za intaneti zikianza kurejea taratibu baada ya kufungwa kwa siku sita wakati wa maandamano makali yaliyoanza siku ya uchaguzi.
Watumiaji wa simu za mkononi wamepokea ujumbe mfupi Jumatatu usiku ukisema kusambaza picha ambazo zinaweza kusababisha hofu au kudhalilisha maisha ya mwanadamu kutapelekea wao kukabiliwa na mashtaka ya uhaini. Ujumbe huo ulitumwa mara tu baada ya intaneti kuunganishwa tena, wakati watu walipoanza kusambaza picha ambazo hazijathibitishwa za miili waliyodai ni ya waathiriwa wa maandamano ya uchaguzi.
Serikali haijatoa mpaka sasa idadi rasmi ya vifo kutokana na maandamano hayo, lakini Rais Samia Suluhu Hassan, wakati wa kula kiapo cha urais Jumatatu, alikiri kuwa watu waliuawa na akavitaka vyombo vya usalama kuhakikisha hali ya kawaida inarejea nchini. Shirika la Human Rights Watch limelaani leo ukandamizaji na matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji nchini Tanzania. Limetaja maafisa kutoka chama kikuu cha upinzani – CHADEMA, waliosema kuwa zaidi ya watu 1,000 wameuawa kwenye maandamano hayo.