
Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, amewasifu raia wa nchi yake kwa uvumilivu licha ya miongo karibu mitatu ya vita, watuj kuuawa na wengine kukosa makazi, kauli anayotoa wakati huu akijaribu kutafuta suluhu na waasi wa AFC/M23 wanaokalia jimbo la Kivu Kaskazini.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika hotuba yake, Tshisekedi aliwasilisha mageuzi yaliyofanywa na nchi yake ili kuondoa umaskini na kukuza ushirikishwaji wa kijamii ,mageuzi hayo yakiwa ni pamoja na Huduma ya afya kwa wote,Elimu ya msingi bila malipo na mipango ya maendeleo kwenye maeneo 145.
Tschisekedi amesema Mipango hii inalenga kuimarisha haki ya kijamii na kuboresha hali ya maisha ya watu, hasa katika maeneo ya mashariki mwa DRC yaliyoharibiwa na vita na migogoro ya mara kwa mara
Viongozi mbalimbali ulimwenguni wanakutana mjini Doha, Qatar katika mkutano wa pili wa maendeleo ya dunia lengo likiwa kushughulikia mapungufu na changamoto zinazoendelea katika jamii, kwa kuzingatia ahadi zilizotolewa katika Azimio la Copenhagen la 1995.