Shirika la kimataifa la Save The Children, linasema mtoto mmoja kati ya watano duniani waliishi katika maeneo yenye mizozo mwaka uliopita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake, shirika hilo lilithibitisha kuwa watoto milioni 520 walikabiliwa na matukio ya kivita mwaka wa 2024, idadi ambayo ilikuwa ya juu zaidi kwa kipindi cha miaka mitatu mfulilizo.

Kulingana na Save the Children, haki za watoto zaidi ya Elfu 40 zilikiukwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 kutoka mwaka wa 2023.

Aidha limesema watoto 78 walikabiliwa na ukiukaji mkubwa wa haki zao, baadhi wakiuawa, kuumizwa, kutekwa, kusajiliwa kwa nguvu kwenye makundi mbalimbali au kudhulimiwa kimapenzi kila siku.

Kulingana na Save the Children, haki za watoto zaidi ya Elfu 40 zilikiukwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 kutoka mwaka wa 2023.
Kulingana na Save the Children, haki za watoto zaidi ya Elfu 40 zilikiukwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 kutoka mwaka wa 2023. © Oxfam France

Afrika ina asilimia kubwa ya watoto ambao wanaishi katika maeneo yenye mizozo ambapo kwa sasa watoto Milioni 218 wako kwenye maeneo yenye mizozo, idadi hiyo ikiipiku ile ya mashariki ya kati kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2017.

Nusu ya ukiukaji wa haki za Watoto duniani uliripotiwa katika maeneo ya Palestine, DRC, Nigeria na Somalia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *