Katika kile kinachotafsiriwa kuwa ni mzozo wa kisiasa, rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ametangaza kumfuta kazi Waziri wake wa fedha, ikiwa ni miezi miwili kupita tangu ateuliwe kwenye wadhifa huo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Athian Diing Athian, ambaye alikuwa amehudumu kama Waziri wa fedha tangu Agosti 2025, alibadilishwa na Barnaba Bak Chol, ambaye alikuwa amefutwa kazi hapo awali kutoka wadhifa huo huo mwezi Machi 2024.

Hakuna sababu rasmi iliyotolewa kwa mabadiliko hayo ya hivi karibuni, ingawa yanakuja kufuatia changamoto kali za kiuchumi nchini humo, ikiwa ni pamoja na mfumuko wa bei wa juu na kushuka kwa thamani ya sarafu.

Mabadiliko hayo yanakuja wakati ambapo masuala ya kiuchumi ya Sudan Kusini yamekuwa mabaya zaidi kutokana na usumbufu wa usafirishaji wa mafuta ghafi unaosababishwa na vita vinavyoendelea katika nchi jirani ya Sudan. Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, limetabiri kushuka kwa uchumi kwa asilimia 4.3 na mfumuko wa bei wa asilimia 65.7 kwa mwaka wa 2025.

Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Riek Machar
Rais Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Riek Machar AFP – PETER LOUIS GUME

Kuondolewa kwa mawaziri ni sehemu ya mtindo wa Rais Kiir wa kufanya mabadiliko ya mara kwa mara katika baraza la mawaziri na jeshi, ambapo wachambuzi wanapendekeza yanalenga kudumisha udhibiti wakati nchi inapokabiliwa na ukosefu mpana wa utulivu wa kisiasa na kiuchumi.

Ukosefu huu wa utulivu unajumuisha kesi inayoendelea ya Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar, ambayo imezua hofu ya kuzuka upya kwa vita. Uchaguzi umesogezwa mbele mara mbili, hivi karibuni zaidi hadi Desemba 2026

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *