Serikali ya Afrika Kusini, imesema imepokea simu za malalamiko kutoka kwa raia wake 17 ambao wamejiunga kwenye kikosi cha mamluki wanaopigana kwenye vita kati ya Urusi na Ukraine.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema, raia hao wa Afrika Kusini ni wanaume wenye umri kati ya miaka 20 na 39 na wamekwama kwenye jimbo la Donbas nchini Ukraine.

Rais Ramaphosa, ameagiza uchunguzi wa kina kuhusu ni vipi, raia hao wa Afrika Kusini, waliingizwa kwenye kikosi hicho cha mamluki.

Hata hivyo, ripoti za awali zinaonesha kuwa haijawa wazi ni upande gani raia hao wa Afrika Kusini, wanapigania katika vita hivyo kati ya Urusi na Ukraine.

Msemaji wa serikali, Vincent Magwenya, amesema tayari serikali ya Afrika Kusini, imeanza jitihada za kidiplomasia ili kuwarejesha nyumbani, huku ikibainika kuwa raia wake 16 wanatokea KwaZulu-Natal, kutoka mkoa wa Cape Mashariki.

Kwa mujibu wa sheria za Afrika Kusini, ni kosa kwa raia wa nchi hiyo kuwa mamluki katika kikosi cha nchi nyingine, bila ya idhini ya serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *