Rais wa Camerun Paul Biya, mwenye umri wa miaka 92, ameapishwa mnamo Novemba 6, 2025, kwa muhula wa nane.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo ambaye ameiongoza Cameroon tangu mwaka 1982 ameapishwa kwa muhula mwingine wa miaka saba wakati wa sherehe katika Bunge la taifa huko Yaoundé. 

Alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Oktoba 12 kwa asilimia 53.66 ya kura, kulingana na matokeo rasmi yaliyochapishwa na Baraza la Katiba. 

Matokeo haya yanapingwa na Issa Tchiroma Bakary, ambaye alishika nafasi ya pili na kudai ushindi. Bakary alikuwa amewataka watu kufanya mgomo wa kususia shughuli kwa siku tatu kuanzia Novemba 3 hadi 5.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *