
Kulingana na mamlaka ya hali ya hewa ya Vietnam kimbunga Kalmaegi kilichoambatana na upepo mkali kimeezua mapaa ya nyumba na kimesomba miti na kuangusha minara ya mawasiliano.
Watu 260,000 wahamishwa kwa usalama wao kupisha kimbunga
Kutokana na janga hilo viwanja sita vya ndege vimefungwa wakati serikali imesema watu 260,000 wamehamishwa kutoka katika mkoa wa Gia Lai na kuwekwa katika maeneo yenye usalama. Pia, wanajeshi 268,000 wamewekwa tayaei kwa ajili ya operesheni za uokoaji na kuwatafuta waathiriwa wa kimbunga hicho.