Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku ya Alhamisi, Novemba 6, kwamba Jeshi la Kimataifa litatumwa “hivi karibuni” kwenda Gaza, siku moja baada ya Marekani kutangaza rasimu ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalokusudiwa kuunga mkono mpango wa amani wa rais wa Marekani. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Hivi karibuni sana. Jeshi litatumwa hivi karibuni. Na mambo yanaendelea vizuri Gaza,” Donald Trump amejibu swali la mwandishi wa habari kuhusu kutangazwa kwa kikosi kama hicho katika eneo la Palestina, ambalo bado linakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu karibu mwezi mmoja baada ya makubaliano ya amani kati ya Israel na Hamas kuanza kutumika.

Balozi Mike Waltz amewaita wajumbe kumi waliochaguliwa wa Baraza siku ya Jumatano, pamoja na washirika kadhaa wa kikanda (Misri, Qatar, Falme za Kiarabu, Saudi Arabia, na Uturuki), kulingana na ujumbe wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa, akibainisha kuwa hii ilionyesha “uungaji mkono wa kikanda” kwa nakala hiyo. Kulingana na vyanzo vya kidiplomasia, nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Indonesia, tayari zimeonyesha nia yao ya kushiriki katika Kikosi cha Kimataifa cha Kuimarisha Udhibiti wa Gaza (ISF), lakini wanasisitiza agizo la Baraza la Usalama la kupeleka wanajeshi katika eneo la Palestina. Kikosi hiki kimeainishwa katika makubaliano yaliyopeekea kusitisha mapigano kwa muda mfupi mnamo Oktoba 10, baada ya miaka miwili ya vita vikali vilivyosababishwa na mashambulizi ya Hamas.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *