
Waathiriwa wa shambulio la bomu kwenye ubalozi wa Marekani nchini Kenya mnamo mwaka 1998 wanasema wamekataa tamaa baada ya uamuzi wa mahakama kuahirishwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu jijini Nairobi, Gaëlle Laleix
Mnamo Agosti 1998, kundi la magaidi Al Qaeda walifnaya shambulio baya katika jengo la ubalozi wa Marekani katikati mwa jiji la Nairobi, na kuua watu 213. Wengi wa walionusurika na familia za waathiriwa nchini Kenya hawajapokea fidia. Mnamo mwaka 2021, waliwasilisha kesi ya kuilazimisha serikali ya Kenya kuomba fidia kutoka Washington. Hukumu hiyo ilitarajiwa Novemba 6, lakini ilihirishwa.
Kwa kuzingatia ukubwa wa kesi hiyo, jaji anabainisha hakuwa na muda wa kutosha kuichunguza ipasavyo. Hoja hii inamkasirisha Douglas Sidialo, ambaye alipoteza uwezo wa kuona katika shambulio hilo nchini Kenya. “Hivi ni visingizio,” anapinga. Kudai kesi hiyo ni kubwa sana haikubaliki! Nani yuko nyuma ya kisingizio hiki? Tumekuwa tukisubiri hukumu hii kwa miaka mingi! Sisi Wakenya hatujawahi kupokea fidia. Kwa nini tunabaguliwa na serikali za Kenya na Marekani?”
Justus Kimathi ni kiongozi wa Muungano wa Waathiriwa wa Agosti 7, 1998. Kwake, hakuna shaka kwamba kesi hii ni ya kisiasa, hasa kwa kuwa Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance anatarajiwa jijini Nairobi mwishoni mwa mwezi. “Ninaamini kwa dhati kwamba hawataki kutoa hukumu kabla ya kuwasili kwa makamu wa rais wa Marekani,” anasema. “Hatuombi serikali ya Kenya itufidie. Ni jukumu la Marekani kufanya hivyo. Walilipa waathiriwa wa Marekani, kwa nini wasifidie mateso ya Wakenya?”
“Hata serikali yetu haijawahi kutaka kukiri yaliyotupata.” Ruth Githuji alimpoteza mama yake katika shambulio hilo. Ilibidi aache shule ili kuisaidia familia yake. Ana matumaini makubwa kwa uamuzi huu. “Ni muhimu kwa sababu hata serikali yetu haijawahi kutaka kukiri kilichotupata,” anasema. “Wanajifanya kama shambulio hilo halijawahi kutokea. Hatukuenda shuleni. Baadhi yetu tunajifanya makahaba ili kula na kuishi. Lakini serikali, haituambii chochote, haifanyi chochote.”
Marekani imewalipa fidia waathiriwa wa Marekani na wafanyakazi wa ubalozi pekee. Zaidi ya manusura 5,000 wa Kenya na ndugu wa waathiriwa wamejiunga na malalamiko ya watu wengi. Uamuzi huo unatarajiwa Januari 15.