
Mkoa wa pwani wa Binh Dinh kusini mwa nchi Vietnam ni miongoni mwa maeneo yalioathirika zaidi.
Umeme umeripotiwa kukatika kwa kiasi kikubwa, miti kung’olewa na safari nyingi za ndege kufutiliwa mbali. Huduma za reli pia zilitatizwa. Mamlaka zimewataka watu kusalia majumbani mwao.
Tahadhari ya mvua kubwa yatolewa
Wataalamu wa hali ya hewa pia wameonya kuweko kwa mvua kubwa na uwezekano wa mafuriko katika siku zijazo.
Kalmaegi ni kimbunga cha 13 kupiga nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia mwaka huu.
Kwa mujibu wa mamlaka ya kukabiliana na majangan ya Ufilipino, idadi ya waliofariki kutokana na Kimbunga Kalmaegi katika siku za hivi karibuni imefikia watu 188.