Maafisa wa Marekaniwamesema safari za ndege zimeahirishwa huku wasafiri milioni 3.2 wakiathirika na hatua hiyo,  kutokana na uhaba wa wafanyakazi, baada ya serikali kutowalipa mishahara yao kufuatia kufungwa kwa shughuli za serikali.

viwanja vya ndege vya Dallas na Austin vimeathirika pakubwa. Takriban safari 2,900 za ndege zimeahirishwa. Hatua nyengine kama hizo zinatarajiwa kuchukuliwa katika viwanja vya ndege vya Houston na Washington.

Kufungwa kwa shughuli hizo za serikali kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Marekani, kumesababisha pia mamilioni ya raia wa taifa hilo wanaotegemea msaada wa chakula kutoka kwa serikali kukosa msaada huo muhimu. 

Wamarekani milioni 4 waachwa bila chakula

Katika jimbo la Minnesota, ambako asilimia 7 ya wakaazi wake wanategemea msaada huo, athari ya kufungwa kwa shughuli za serikali ni kubwa, huku jamii ikishirikiana kuziba pengo na kuwasaidia watu walio na mahitaji. Hali hiyo Marekani, imetokana na mvutano wa masuala ya bajeti kati ya vyama vya Republican na Democratic.

Kwa mamilioni ya wamarekani kadi ya chakula ya SNAP inamaanisha chakula mezani, lakini mfumo kwa sasa umeacha kufanya kazi, kwahiyo chakula hicho hakipatikani. App ya SNAP katika simu ya raia mmoja kwa jina Mary, inaonesha fedha alizobakiza katika app hiyo. Tangu rais wa Marekani Donald Trump alipofungia app hiyo, hakufanikiwa kuingiziwa fedha zozote mwezi huu.

Mapngo huo wa kuwasaidia watu kupata chakula, unawapiga jeki takriban watu 430,000 katika jimbo la Minnesota na kitaifa, wamarekani milioni 4 wanaitegemea. Hakuna mtu anaejua hadi sasa Marekani itabakia katika mkwamo huo kwa muda gani. Wamarekani sasa hawawezi kuitegemea serikali kupata chakula kwahiyo wanategemeana kupata chakula hicho.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *