Paul Biya wa Cameroon, ambaye ndiye Rais mwenye umri mkubwa zaidi duniani, ameapishwa kwa muhula wa nane kuwa Rais wa nchi hiyo siku ya Alhamisi, baada ya uchaguzi wenye utata uliochochea maandamano.

Katika hotuba yake ya kuapishwa, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 92 ameahidi kurejesha utulivu katika taifa hilo la Afrika ya Kati na kuwalaumu wanasiasa wasio na uwajibikaji pamoja na raia wanoishi nje ya nchi kwa kuchochea vurugu.

“Napochukua madaraka, natambua kwa kina uzito wa hali ambayo nchi yetu inapitia. Natambua wingi na ukali wa changamoto tunazokabiliana nazo. Natambua kina cha hali ya kukata tamaa na ukubwa wa matarajio ya wananchi,” Biya aliwaambia waliokuwa wakimsikiliza.

Kulingana na taarifa kutoka vyanzo viwili vya Umoja wa Mataifa, vikosi vya usalama viliwaua raia 48 wakati wa maandamano dhidi ya kuchaguliwa tena kwa Biya. Serikali haijatoa taarifa wala kutoa makadirio yake kuhusu idadi ya waliouawa au kujeruhiwa katika machafuko hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *