
Wasiwasi unaendelea kuongezeka kuhusu ukubwa wa ukatili unaofanywa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika jiji la El-Fasher, ambalo sasa linakabiliwa na hali ngumu ya kibinadamu. Ingawa picha za setilaiti zinashuhudia mauaji yaliyotokea huko, wapiganaji wa Jenerali Hemedti wenyewe wanachapisha video kwenye mitandao ya kijamii ambapo wanaonekana wakijipanga na kufanya uhalifu mwingi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wasiwasi unaongezeka nchini Sudan kuhusu kinachoendelea El-Fasher. Zaidi ya siku kumi tu baada ya jiji kutekwa na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), kundi la wanajeshi wa Jenerali Hemedti, jiji hili limetengwa kabisa na ulimwengu: huku mawasiliano na jiji hili yakikatwa, picha za setilaiti zinaonyesha miili mingi na makaburi ya watu wengi.
“Tuna wasiwasi mkubwa,” anasema Altahir Hashir, raia wa Sudan kutoka diaspora na sehemu ya mtandao wa usaidizi wa pande zote na El-Fasher. “Hatujui kinachoendelea huko: kunaripotiwa hali ya sintofahamu, hali ni nzito katika jiji hili. Umoja wa Mataifa unasema ulikuwa na wakaezi 250,000. Ikiwa watu 70,000 wanliweza kutoroka mji huo, nini kilitokea kwa watu wengine?” anaongeza. “Tulikuwa tukiwasiliana na wakazi, wanachama wa mashirika ya kiraia, madaktari, watu wa kujitolea, watu waliofanya kazi katika madhirika mbalimbali, na hatuna habari yoyote kutoka kwao: wametoweka kabisa. Hii ni kweli hasa kwa madaktari waliofanya kazi katika hospitali ya Saudi Arabia: hatujui kama bado wako hai au la.” “Kama tulivyoona video kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha ndani ya hospitali ambapo wanajeshi walikuwa wakiwaua kila raia, kwa bahati mbaya ninaogopa kwamba baadhi yao wanaweza kuwa wameuawa,” Altahir Hashir amesema, bado akiwa na wasiwasi.
Video nyingi ambazo wanajeshi wanaonyeshwa wakifanya ukatili mbaya zaidi zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii. Miongoni mwa video hizi, moja inaendelea kuonyesha: ile ya kamanda wa FSR akiwakabili raia wakiwa wamepiga magoti, akionekana kuwa na hofu. Akihutubia, anacheka, anawadhihaki, kisha anawapiga risasi. Picha hizi zilizoruhwa kwenye akaunti yake ya TikTok, ambayo ina wafuasi 20,000, ni wazi zimesababisha hasira.