Video ya UNICEF umeonesha lori lililojaa mabox yenye rangi ya kaki ambayo yana nembo ya buluu ya UNICEF watu wanayashushwa chini maboxi hayo, kisha watoto wanaonekana wakiandika katika karatasi na kisha kupewa begi, wanayavaa mgongoni. Watoto wawili wa kike wakiwa wameyavaa mabegi yao wanashikana miwili na kuruka ruka nyuso zao zimejaa furaha.

Video inamuonesha mtoto mmoja wa kiume anatembea akiwa amebeba begi la buluu lenye nembp ya UNICEF na Muungano wa Ulaya, anafika nyumbani kwao, mama yake amekaa jikoni na ungo akichambua nafaka, mtoto anafungua begi na kumuonesha yaliyomo ndani ya begi hilo alilopewa anamwambia huku anatoa kimoja baada ya kingine… tumepewa penseli, peni, madaftari, rula, ufutio na vitu vingine vingi. Kisha anafunga begi lake na kulitundika juu kwenye msumari. Mama na mwana wanafuraha.

Katika eneo la Asgede wilayani Woreda huko Tigray UNICEF na Muungano wa Ulaya wametoa mabegi hayo ya msaada kwa watoto 11,500 kati yao zaidi ya 6,000 wakiwa ni watoto wa kike.

Tadesse Tesfaye Abraham, mvulana mkali mwenye umri wa miaka 13 kutoka kaskazini-magharibi mwa Tigray.

UNICEF / Mulugeta Ayene

Afework Gebrehiwot ni meneja wa masuala ya ulinzi wa watoto,elimu na masuala ya kibinadamu anasema ’Lengo la usambazaji huu ni kuhakikisha watoto wanaweza kwenda shule. Kwasababu ya changamoto za kiuchumi na nyingine nyingi, wazazi walishindwa kuwanunulia watoto wao mabegi.”

Watoto wanaeleza furaha zao. Huyu ni Andom Teklit mkimbizi wa ndani ambaye familia yake ilikimbilia Mayhansse, …. Hapa anasem shule ni muhimu kwa kila mtoto. Anapenda sana shule kwasababu inamsaidia asitumbukie kwenye tabia mbaya na hilo ni jambo muhimu kwake.

Mbali na msaada wa mabegi UNICEF na Mungano wa Ulaya wanatoa usaidizi kwa kuwapa mafunzo walimu, kufanya kampeni za kuhamasisha watoto kurejea shuleni, msaada wa kisaikolojia na kijamii na kununua samani / furniture yote haya katika kuhakikisha watoto wanarejea shuleni kusoma baada ya kipndi kirefu cha vita katika eneo la Tigray.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *