Ni tuzo inayojulikana kama Tuzo ya Afrika ya Ujerumani 2025. Namatai Kwekweza amepongeza Ujerumani kwa tuzo hiyo akiitaja ushahidi wa uhalali wa kile ambacho amekuwa akikipigania.

“Wakfu wa German Africa Foundation umenipatia tuzo hii kwa ajili ya uaminifu wake wa kuunga mkono utawala wa sheria na demokrasia nchini mwangu.” Alisema Kwekweza.

Kwekweza, ambaye ana umri wa miaka 26, ni mwanzilishi wa WELEAD Trust, shirika alilolianzisha akiwa na miaka 18 ili kuandaa vijana viongozi na kuwashirikisha katika maamuzi ya kisiasa.

Katika harakati hizo za utetezi wa demokrasia, haki na utawala shirikishi kwa vijana Kwekweza amekumbana na hali ngumu ikiwemo kukamatwa mara kadhaa na kupelekwa jela, kuonywa, na mara nyingi kuwekewa vitisho hadharani kwa lugha za kukosewa heshima na watawala wa Zimbabwe.

: Mapambano ya demokrasia ni magumu

Kwekweza pia ameiambia DW kuwa mapambano kwa ajili ya ukweli ni magumu lakini ni ya lazima.

Akizungumzia jitihada zake hizo Kwekweza alisema “kila mafanikio yanakuja na gharama.” Aliongeza: “Kama unachukiwa kwa kusema ukweli mbele ya wenye madaraka, au ukiwekwa ndani kwa kusema ukweli ni ngumu. Lakini pia ni ngumu kuiishi maisha ambayo yamepungukiwa na fursa na uwezekano.”

Jopo la watu 20 lilimchagua Kwekweza miongoni mwa wagombeaji zaidi ya ishirini kwa sababu ya ujumbe wake wa kujiamini na uamsho wa kidemokrasia.

Yvonne Aki Sawyerr ashinda Tuzo ya Ujerumani kwa Afrika

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Mwenyekiti wa jopo hilo, Claus Stäcker, alielezea namna Kwekweza anavyowakilisha mfano mzuri wa harakati za vijana wa kizazi kipya maarufu kama GenZ katika nchi za Kenya, Tanzania, Madagascar na Cameroun ambapo. vijana hao wanaendelea kupambana kudai mabadiliko katika demokrasia, uwazi kwenye utawala na huduma nzuri za kijamii na kiutawala.

Kwekweza pia ameitaja tuzo hiyo kama isiyokuwa kama heshima kubwa ambayo hakuitegemea na yeye pia kuitunukia shirika lake hilo lake hilo la WELEAD na vijana wenzake wanaoshirikiana kwenye harakati hizo. Kwa kauli yake anadhani tuzo hiyo itaweka hamasa na nuru mpya kwa wanaharakati vijana wa demokrasia nchini Zimbabwe.

Je, Tuzo ya Afrika Ujerumani ina maana gani?

Tuzo ya Afrika ya Ujerumani ni heshima ya hali ya juu sana, ikitolewa tangu mwaka 1993 na German Africa Foundation taasisi isiyo ya kisiasa inayoakisi sura ya kina ya demokrasia ya Afrika ndani ya medani za kisiasa nchini Ujerumani.

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz
Kansela wa Ujerumani Friedrich MerzPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Tuzo hii hutolewa kwa wanaharakati barani Afrika waliotoa mchango wa kipekee hasa katika kupigania demokrasia, haki za binadamu,amani, maendeleo endelevu, utamaduni na sanaa pamoja na masuala ya kijamii.

Washindi wa zamani waliowahi kupewa tuzo hiyo ni pamoja na meya wa Freetown nchini Sierra Leone Yvonne Aki-Sawyerr, watafiti virus vya janga laCOVID-19 Tulio de Oliveira na Sikhulile Moyo, na viongozi watetezi wa haki za binadamu kama Waris Dirie na Ilwad Elman pamoja na Rais wa zamani wa Botswana Ketumire Masire na wana harakati wa  Somalia Waris Dirie and Ilwad Elman.

Tuzo hii ya Kwekweza itawasilishwa rasmi tarehe 26 Novemba 2025 na Julia Klöckner, Spika  wa bunge la Ujerumani Bundestag.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *