
Kupitia jarida la Wall Street la Marekani, Al Burhani ambaye jeshi lake linapambana na wanamgambo wa RSF amesema watu wa Sudan sasa wameweka matumaini yao kwa Marekani kuchukua hatua inayofuata ili kurejesha amani.
Wiki iliyopita, Trump alionesha nia ya kuingilia kati katika vita hivyo baada ya kuombwa na Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed Bin Salman kusaidia kuvitatua.
Mapigano yawaondoa wafanyakazi wa MSF kwenye hospitali Darfur
Katika hatua nyingine, Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka MSF limesema lililazimika kuwaondoa wafanyakazi wake kutoka katika hospitali moja mjini Darfur baada ya muhudumu mmoja wa afya kupigwa risasi na kuuawa.
Mtu huyo aliyekuwa mfanyakazi wa wizara ya afya aliuawa kwa kupigwa risasi ndani ya hospitali ya Zalingei Novemba 10 na watu wengine wanne walijeruhiwa.