Jeshi limetangaza pia kuifunga mipaka yote ya nchi hiyo, kumtia mbaroni rais Embalo na maafisa wengine pamoja na wanasiasa wa upinzani ikiwa ni pamoja na Fernando Dias na Waziri Mkuu wa zamani Domingos Simoes Pereira.

Mapinduzi hayo yamejiri wakati tume ya uchaguzi inatarajiwa siku ya Alhamisi kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais uliokuwa na ushindani mkali ambapo pande zote mbili zinadai kushinda. Jeshi la  Guinea-Bissau  limetangaza pia kusitisha mchakato wa uchaguzi na kutangaza amri ya kutotoka nje.

Jumuiya ya kimataifa imetoa wito wa kujizuia na kuheshimu mchakato wa kidemokrasia katika nchi ambayo imepitia mapinduzi mengi ya kijeshi tangu ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa Ureno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *