Washirika wa Ukraine wana wasiwasi kwamba utawala wa Trump unaweza kuishinikiza Kyiv kusaini mpango huo wenye vipengee 28  uliotangazwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita.

Mpango huo unaitaka Ukraine kuachia baadhi ya maeneo kwa Urusi, kupunguza idadi ya jeshi lake na kuahidi kutojiunga na Jumuiya ya kujihami ya NATO.

Wakati huohuo, Marekani inaendelea na juhudi za kufanikisha mpango huo wa amani. Katibu Mkuu wa Jeshi la Marekani Daniel Driscoll sasa anafanya mazungumzo na ujumbe wa Urusi huko Abu Dhabi, baada ya kukutana na maafisa wa Ukraine mjini Kyiv.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *