Mkutano wa uzinduzi wa tawi jipya la vijana la chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfDnchini Ujerumani, ulicheleweshwa kwa zaidi ya saa mbili leo baada ya waandamanaji kuzuia njia ya kuingia ukumbini.

Maelfu ya waandamanaji wanaopinga AfD walianza kuwasili katika mji wa kati wa Giessen karibu na Frankfurt kuanzia asubuhi na mapema, huku polisi pia wakiwa nje. Moja ya mashirika yaliyoratibu maandamano la Resist, limesema kwamba lilizuia njia kadhaa kuelekea mkutano huo na kiasi cha watu 15,000 walikusanyika.

Kiongozi mwenza wa chama hicho Alice Weidel, amelaani ghasia hizo na kusema wale waliokusanyika ukumbini walikuwa ni kizazi kipya cha chama.  Tawi jipya la vijana litachukua nafasi ya Junge Alternative (JA), ambalo liliorodheshwa kama kundi lenye msimamo mkali na kisha kufutwa na AfD mapema mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *