Kamanda Mkuu wa Jeshi amesema, Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeshajiweka tayari kikamilifu kutoa jibu kali kwa tishio lolote dhidi ya maslahi yake ya taifa, na kusisitiza kwamba mkakati wa ulinzi wa Iran umejengwa juu ya msingi wa kuzuia hujuma.

Meja Jenerali Amir Hatami ameyasema hayo leo katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha vyombo vya majini cha Kordestan na kuongezwa manowari ya mashambulizi ya Sahand kwenye manowari za kusini za vikosi vya Wanamaji vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na akasisitiza kwa kusema: “mkakati wetu wa ulinzi umejengwa juu ya ulinzi amilifu na uzuiaji erevu wa hujuma.”

Jenerali Hatami ameongezea kwa kusema: “hii inamaanisha kwamba hatutasubiri adui ashambulie, na tuna utayari unaohitajika wa kutoa mjibizo mkali na wa kusambaratisha popote pale yanapohitaji maslahi yetu ya taifa”.

Sambamba na kuuenzi moyo wa kujitoa mhanga wa vikosi vya Wanamaji vya Jeshi wakati wa vita vilivyoanzishwa na Iraq dhidi ya Iran, Kamanda Mkuu wa Jeshi amesema, nguvu za Iran zinabaki kuwa za kuleta uthabiti na utulivu kwa taifa na eneo pana.

“Leo, mtu hawezi kutofautisha kati ya usalama wa eneo na usalama wa nchi za eneo”, amefafanua Jenerali Hatami.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran amebainisha kuwa uzoefu wa karibu miongo mitano wa tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 umedhihirisha “nafasi na mchango usio na mbadala wa ujengaji wa Iran” kwa usalama wa kikanda, na akaongeza kuwa matukio yaliyojiri katika miaka miwili iliyopita yameweka wazi ni nchi zipi zinazovuruga usalama wa kikanda, na kutobakisha shaka yeyote kwa kila mtazamaji mwenye insafu…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *