Mkutano Mkuu wa Simba wa mwaka 2025, umeisha saa 5:59 asubuhi, huku ukiibua maswali kwa wanachama kutokana na jinsi ulivyomalizika.

Mkutano huo ambao awali ulihudhuriwa na wanachama 720, kisha baadaye kuongezeka hadi 998, umemalizika huku wanachama hao wakiwa hawajui mustakabali wa yale yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho kwenye katiba.

Hatua hiyo imejiri baada ya mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba yalivyomalizwa kusomwa, ambapo ghafla Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu alitangaza mkutano huo kumalizika.

Baada ya hatua hiyo, ndipo pakaibuka sintofahamu kwa wanachama waliodai kudharauliwa na Mangungu na kumtaka ajiuzulu mara moja kwa kumaliza mkutano huo bila kujadili jambo muhimu lililowaleta.

“Tumekuja hapa kufanya nini? Mwenyekiti huyo vipi mbona yale mapendekezo hatujayajadili hii siyo sawa hata kidogo, kilichotuleta hatujakijadili sasa ni nini hii, mwenyekiti anatakiwa kujiuzulu haraka,” alisema mmoja wa wanachama wa timu hiyo.

Baada ya huyo, wanachama wengine kwa umoja wao, walipiga kelele kwa sauti wakimtaka ajiuzulu, huku wakidai sababu za timu kufanya vibaya kwa  ni kutokana na hali iliyojitokeza leo kwenye mkutano huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *