Kiongozi wa kisiasa na kiongozi wa chama cha Manidem, Anicet Ekane, amefariki usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu, Desemba 1, kulingana na wanasheria wake na familia yake asubuhi ya leo. Ekane alikamatwa Oktoba 24 huko Douala na tangu wakati huo alikuwa amezuiliwa katika Sekretarieti ya wizara ya Ulinzi huko Yaoundé.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na wanasheria wake, afya ya Ekane ilizorota wikendi nzima, licha ya huduma aliyokuwa akipokea katika kambi ya kijeshi. Siku ya Jumapili, Novemba 30, chama chake cha siasa, Manidem, kikiwa na wasiwasi na kuzorotakwa afya ya kiongozi wake, kilitoa taarifa kikitaka uhamisho wake wa haraka kwenda hospitali nyingine kwa ajili ya huduma ya matibabu ambayo ilitarajia ingekuwa “muhimu na inayofaa zaidi.”

Taarifa hiyo imetangaza kwamba chama hicho “kitawajibisha utawala wa Yaoundé kwa matokeo ya kukataa uhamisho huu,” ambao kiliutamani kwa dhati. Asubuhi ya leo, habari hizo zilisambaa ghafla, zikithibitishwa na familia yake na mawakili wake: Anicet Ekane amefariki kizuizini, siku 38 baada ya kukamatwa kwake huko Douala, siku moja baada ya uchaguzi wa rais.

Akiwa mtu maarufu katika maisha ya umma na kisiasa nchini Cameroon, tangazo la kifo chake tayari limezua hisia nyingi. Baadhi ya vyombo vya habari vya ndani vilikatiza vipindi vyao ili kutangaza ripoti za moja kwa moja, na kwenye mitandao ya kijamii, jumbe za maombolezo na rambi rambi zimeendelea kumiminika. Anicet Ekane alikuwa mtu anayeongoza katika uwanja wa kisiasa nchini Cameroon. Amekuwa akihusika katika kila mapambano makubwa ya umma na kisiasa tangu mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Mwaka huu tena, mwaka wa 2025, alichukua jukumu muhimu katika mchakato wa uchaguzi wa rais uliomalizika hivi karibuni. Kwanza, kwa kumuunga mkono Maurice Kamto chini ya bendera ya chama chake, Manidem. Kisha, kwa kutoa msaada wake kamili kwa Issa Tchiroma Bakary, ambaye alitangazwa kuchukuwa nafasi ya pili katika uchaguzi huo lakini anadai ushindi.

Akiwa mfuasi hai wa Issa Tchiroma Bakary, alishutumiwa, pamoja na viongozi wengine, kwa uasi baada ya kutambua ushindi wa ‘Issa Tchiroma Bakary katika uchaguzi wa urais. Matokeo rasmi, yaliyomtangaza Paul Biya kuwa mshindi, yanapingwa na sehemu ya upinzani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *