Jumuiya ya ECOWAS inatuma ujumbe wake kwenda nchini Guinea Bissau, msafara ambapo msafara huo utaongozwa na mwenyekiti wa sasa wa jumuiya hiyo rais wa Sierra Leone, Julius Maada Bio, kujaribu kupata suluhu ya mzozo wa kisiasa kwenye taifa hilo ikiwemo kurejea kwa utawala wa kikatiba.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais Bio ataambatana na viongozi wengine kutoka Senegal, cape Verde na Togo, ambapo jukumu lao kubwa litakuwa ni moja tu, kuelewa kilichofanyika pamoja na uwezekano wa kuwashawishi wanajeshi kurejesha utawala wa kiraia hata kabla ya mwaka mmoja waliojipea.

Ziara hii inafanyika wakati ambapo tayari umoja wa Afrika mwishoni mwa juma lililopita, ulitangaza kuisimamisha Guinea Bissau uanachama, ECOWAS nayo ikitishia kuchukua hatua kama hizo ikiwa wanajeshi hawataheshimu maelekezo yao.

Juma lililopita kiongozi wa mpito wa kijeshi, Horta N’Tam, alitangaza baraza la mawaziri la watu 28, akisema litamsaidia kuongoza kwa mwaka mmoja kuelekea kurejesha utawala wa kiraia.

Haya yanajiri wakati huu aliyekuwa rais w anchi hiyo, Umaro Sissoco Embalo, mwishoni mwa juma lililopita, aliwasili nchini Congo Brazzaville ambako amepatiwa hifadhi ya kisiasa akitokea Senegal alikokimbilia mara ya kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *