Serikali ya Ethiopia imezindua Mkakati wa Kidijitali wa Ethiopia 2030, unaolenga kukuza matumizi ya teknolojia katika sekta zote za kiuchumi na kuugeuza uchumi wa nchi hiyo ya Pembe ya kuwa wa kidijitali kikamilifu.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Ethiopia imetoa taarifa na kusema: Baraza la Mawaziri la Ethiopia ambacho ni chombo kikuu cha utendaji cha nchi hiyo, limeidhinisha mkakati wa kitaifa wa mabadiliko ya kidijitali wa miaka mitano ili kuharakisha ukuaji wa uchumi na kuboresha huduma za umma.

Mkakati huo unalenga kuimarisha uwezo wa kiteknolojia wa Ethiopia, kustawisha miundombinu muhimu na kuleta fursa mpya za kijamii na kiuchumi kwa raia, hasa kwa vijana wanaotafuta ajira na kulitumikia taifa kwa nguvu na damu zao changa.

Mpango huo mpya umeanzishwa kuchukua nafasi ya mkakati wa awali wa kidijitali wa Ethiopia 2025, ambao ulizinduliwa mwezi Juni 2020.

Wizara ya Ubunifu na Teknolojia ya Ethiopia ilisema hivi karibuni kwamba Mkakati wa Kidijitali wa Ethiopia 2025 “umefanikiwa kwa asilimia 100,” na umeweka msingi wa kukuza uchumi wa kidijitali unaoongozwa na teknolojia na unaotegemea maarifa ya kisasa.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amesema: “Kufuatia kukamilika kwa mafanikio Mkakati wa Kidijitali wa Ethiopia 2025, ambao ulilenga kuleta uvumbuzi na kustawishwa sekta mbalimbali kwa kutegemea tekonolojia na maarifa, sasa tumezindua Mkakati wa Kidijitali wa Ethiopia 2030, ambao utaimarisha utoaji wa huduma kupitia matumizi makubwa ya pembejeo za mashine ambazo zinazoendeshwa kwa njia za kiotomatiki.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *