Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Chande Othman ambaye amekuwa na uzoefu na kuendesha tume nyingi za kiuchunguzi ndani na n je ya nchi, amesema tume hiyo iko tayari kufanya kazi na makundi yote na kwamba iwapo upande mmoja wa makundi hayo utaonyesha shingo upande kutoa ushirikiano, tume hiyo itajitahidi kuendelea kuyashawishi lakini iwapo itashindikana basi majukumu yake ya tume yataendelea.
“Kwahiyo tunatoa wito kwa Watanzania, wadau wote, tushirikiane ili tume iweze kupata taarifa sahihi na nasisitiza ya ukweli.”
Kuhusu tume hiyo kuundwa na watu wazima ikiacha kundi kubwa la vijana ambalo ndio chimbuko ya yale yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi, kiongozi huyo aliaondoa wasiwasi akisema kundi hilo linazingatiwa. Alisema watu wazima wazoefu wa mambo lakini jambo hilo halimaanisha vijana wanapuuzwa.
Alisisitiza kuwa tume hiyo itafanya kazi katika maeneo yote ikiwamo kwenda katika maeneo yaliyoathirika na vurumai na kule ambako kulikuwa shwari.
“Wadau wakubwa ni vijana kwa hiyo tutakuwa na mbinu mbalimbali za kuwashirikisha vijana, siyo vijana waliosoma tu, wasiosoma wenye ajira, na wasiona ajira, mazingira gani hawa ni eneo kuwa la kuwa nao.”
Kuhusu kuwepo kwa baadhi ya wajumbe wanaotiliwa shaka hasa jina la Stergomen Tax aliyekuwa Waziri wa ulinzi wakati hali ya mambo ikichafuka, Jaji Chande alisema tume hiyo imeundwa kisheria na wajumbe wake wote wamekula kiapo hivyo watawajibika kutenda haki.
Upinzani bado hauna imani na tume iliyoteuliwa na Rais Samia
Hata hivyo alisema kama hali itathiri kuwa mmoja ya wajumbe kuwa sehemu ya mgongano wa kimaslahi wakati wa kutimiza majukumu yake, tume hiyo itamwomba akae pembeni.
“Tukiona mjumbe yoyote ana conflict of interest ( mgongamno wa kimaslahi), tutamwomba ajitoea na mwenyewe anaweza kujitoa haina teno. Lakini lingine mwelewe kwa maana nasema tume hii ni ya kisheria wote tumekula kiapo na tutajikita kwenye ushahidi ambao tunaridhika nao.”
Tume hiyo iliyotangazwa Novemba 20 imekuwa ni sehema ya majadala mkubwa inayoendelea kutokaa kwa makundi mbalimbali ya wakosoaji ikiwamo vyama vya upinzani vinavyoonesha kukosa Imani nao.
Chama cha upinzani Chadema ni miongoni mwa vyama vilivyojitokeza wazi kupinga tume hiyo na hii leo alipotakiwa na DW kutoa maaoni yake baada ya maelezo ya mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Chande, makamu mwenyekiti wa chama hicho John Heche alisema msamamo wa chama chake bado uko pale pale akitaja pia sababu ya kukosa uwakilishi wa vijana.
“Kwa hiyo serikali haiwezi kujichunguza yenyewe wakati serikali ni mtuhumiwa hivi inaruhusiwaje mtuhumiwa ajichunguze ili aone ana makosa au hana unategemeaje hapo,” alisema John Heche.
Tume hiyo iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hasssan imepewa muda wa siku 90 kukamilisha majukumu yake na kwamba kazi hiyo imeanza kuhesabika tangu Novemba 20.
