Mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyozikumba nchi nne za bara la Asia yamesababisha vifo vya takriban watu 1150, huku idadi hiyo ikiendelea kuongezeka kadri siku zinavyosonga tangu mvua kubwa zianze kunyesha wiki iliyopita.

Athari hizo zimesababishwa na vimbunga Senyar na Ditwah, ikielezwa kuwa nusu ya waliokufa maji wameripotiwa nchini Indonesia, ambako kuna madhara makubwa zaidi ikilinganishwa na mataifa mengine ya Sri Lanka, Thailand na Malaysia.

#Azamtvupdates
Mhariri | @abuuyusuftz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *