Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini jana alimtuhumu Rais Donald Trump wa Marekani kwa kuendelea kutoa “taarifa zisizo za kweli” kuhusu nchi yake.

Akihutubia taifa, Ramaphosa alisema kuwa ametilia maanani kauli ya Trump aliyoitoa siku kadhaa zilizopita kwamba hataialika Afrika Kusini kwenye mkutano wa G20 huko Florida mwakani.

“Trump Amekariri kauli zisizo za kweli kuhusu mauaji ya halaiki dhidi ya Waafrikana na kunyakuliwa ardhi za wazungu nchini kwetu, amesema” Rais wa Afrika Kusini alisema.

Trump alitangaza wiki iliyopita kuwa Afrika Kusini haitaalikwa kwenye mkutano wa kilele wa G20 wa mwaka kesho utakaofanyika Marekani, akitolea mfano madai kwamba nchi hiyo imekataa kukabidhi uenyekiti wa G20 kwa mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani.

Rais Cyril Ramaphosa amesema kuwa mapema wiki hii Afrika Kusini imekabidhi rasmi uenyekiti wa kundi la G20 kwa Marekani kwa ajili ya mwaka ujao na hivyo kuzingatia itifaki stahiki za kidiplomasia.

Trump alisusia Mkutano wa mwezi huu wa G20 uliofanyika wiki jana huko Johannesburrg akidai kuwa Waafrika Kusini wazungu wanauliwa kiholela na wanaporwa ardhi yao, madai ambayo serikali ya Afrika Kusini imeyakanusha na kutataja kuwa hayana halina msingi wowote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *