Serikali imesema itawafutia hadhi ya ukimbizi, wakimbizi 238,956 wanaoishi nchini baada ya nchi zao kurejea kwenye hali ya amani, ambapo awali zilikumbwa na machafuko.
Kauli hiyo ya serikali imetajwa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene kwenye mkutano maalum wa Tanzania, Burundi na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) na kueleza kuwa miongoni mwa wakimbizi hao ni Warundi 152,019, Wakongo 86,256 na kutoka mataifa mengine ni 681.
#Azamtvupdates
Mhariri | @abuuyusuftz