Umoja wa Afrika umesimamisha uanachama wa Guinea-Bissau baada ya mapinduzi ya kijeshi ukisema hautavumilia mabadiliko ya serikali kinyume cha katiba.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baraza la Amani na Usalama la AU limesema nchi hiyo imezuiwa kushiriki shughuli zote za Muungano huo hadi pale utaratibu wa kikatiba utakaporejeshwa.

Hatua kama hii ya AU imechukuliwa pia na jumuiya ya kikanda ya nchi za Afrika Magharibi  ECOWAS.

Makataa ya AU yamekuja wakati huu, Rais aliyeondolewa madarakani Umaro Sissoco Embaló akiripotiwa kuwasili Congo-Brazzaville akitokea Senegal, hii ni kulingana na mkuu wake wa wafanyakazi.

Siku ya Jumamosi, kiongozi mpya anayeungwa mkono na jeshi, Jenerali Horta Inta-a, aliteua serikali ya mpito yenye mawaziri 28.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *