Utekelezaji wa mpango huu unawezekana kutokana na ufadhili wa kifedha kutoka The LEGO Foundation na Hapag-Lloyd, ambao wamejitolea kuhakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma . Wanachokifanya ni kuwapatia watoto vyeti vya ulemavu vinavyowawezesha kupata huduma muhimu zinazotolewa na serikali. Elizabeth Kimani, afisa kutoka Taasisi ya KISE anaeleza kinachoendelea katika zoezi hilo muhimu.

Sasa hivi tuko katika Kaunti ya Wajir kwa siku ya pili. Tunafanya tathmini kwa watoto wenye mahitaji maalum na ulemavu, tukilenga watoto walio nje ya shule na walio ndani ya shule. Lengo letu ni kuwafanyia tathmini na kuhakikisha wanapangwa ipasavyo katika shule ili waweze kupata elimu bora.”

UNICEF na KISE wawafanyia tathmini watoto wenye ulemavu katika Kaunti ya Wajir Kenya ili wapate elimu bora na jumuishi.

UNICEF na KISE wawafanyia tathmini watoto wenye ulemavu katika Kaunti ya Wajir Kenya ili wapate elimu bora na jumuishi.

Baada ya tathmini watoto wanatambuliwa rasmi na wanaweza kufikiwa na msaada wanaouhitaji kukuza uwezo wao kitaaluma, kiafya na kijamii. Bi. Kimani anafafanua zaidi.

“Hapo awali, kabla ya zoezi hili, tuliweza kufundisha walimu ambao walichaguliwa mahsusi kutoka shule hizo. Walipatiwa mafunzo ili waweze kutoa elimu jumuishi katika shule hizo. Iwapo walimu hawana ujuzi na stadi kuhusu jinsi ya kushughulikia wanafunzi walio na uoni hafifu au wasioona kabisa, basi watabaki kuwa watazamaji tu pasipo kuwasaidia ipasavyo, na wanafunzi hao hawataweza kuendelea katika ngazi nyingine za masomo.”

Katika harakati za kuboresha maisha ya watoto hao, tathmini sahihi ndiyo hatua ya kwanza. Kwa ushirikiano wa wadau wakuu wa elimu nchini, juhudi hizi sasa zinafanyika kwa kina na kwa umakini. Elizabeth Waitha ambaye ni Afisa wa Elimu  wa UNICEF Kenya, Anasema

Tathmini ni jambo muhimu sana kwa mtu yeyote mwenye ulemavu, na hasa kwa watoto  Tathmini za mtu mmoja mmoja hutusaidia kubaini ni mahitaji gani yanayohitajika ili kuwaunga mkono watoto hawa. UNICEF, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, Idara ya Elimu Maalum, na Chuo cha Elimu Maalum cha Kenya KISE, wameungana kufanya tathmini ya uwezo wa watoto wenye ulemavu. Hii ni hatua ya mwanzo kabisa ya kubaini aina ya ulemavu pamoja na vifaa vya usaidizi na aina nyingine za msaada wanaohitaji ili waweze kuandikishwa na kuendelezwa shuleni.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *