
Mlima wa volkano katika Mkoa wa Afar nchini Ethiopia, Erta Ale hivi majuzi ulilipuka na kutoa majivu, huku wataalamu wakisema ulikuwa mlipuko wa kwanza wa aina hiyo baada ya zaidi ya miaka 10,000.
Erta Ale ni mojawapo ya maajabu ya asili ya kuvutia zaidi ya bara.
Volkano hii ina ziwa la lava lisilobadilika ambalo limevutia wanasayansi na wavumbuzi. Mazingira magumu ya maajabu haya ya kijiolojia, ambayo mara nyingi hujulikana kama “Lango la Kuzimu,” inaongeza hali yake ya upekee.
Barani Afrika kuna baadhi ya volkano za ajabu zaidi duniani likiripotiwa kuwa na zaidi ya volkano 100 ambazo zinaweza kulipuka wakati wowote.
Tuangazie volkano kadhaa.
Volkano za Tanzania
Mlima Kilimanjaro, uliopo nchini Tanzania pia unajulikana kama ‘Paa la Afrika’.
Una urefu wa mita 5,895, na unatambulika kwa kuwa kilele cha juu zaidi barani Afrika.
Wataalamu wanasema ulilipuka zaidi ya miaka 200,000 iliyopita, na sasa unajulikana kama volkano iliyotulia.
Hapo tu tanzania kuna Mlima Meru, umeripotiwa kuwa na milipuko minne, ambapo mara ya mwisho ulitokea mwaka wa 1910. Kilimanjaro imefunika sifa ya Mlima Meru lakini licha ya hayo, mlima huo unawapa wanaopanda mlima mazingira magunu lakini ya kuridhisha kwa wanaopenda shughuli hizi.
Mlima wa volkano Ol Doinyo Lengai pia unapatikana nchini Tanzania. Miongoni mwa watu wa jamii ya Wamasai, wanauita “Mlima wa Mungu,” wakitoa heshima kwa ubunifu usio na kifani wa asili.
Ol Doinyo Lengai ni wa kipekee kutokana na kuwa volkano yake ni mojawapo ya chache duniani zinazolipuka na lava adimu ya ‘’carbonatite’’.
Mapema Septemba 2007, ililipuka na kusababisha kuwepo kwa wingu la majivu kwenye angahewa.
Milima ya kenya
Nchini Kenya Mlima Kenya, ina kilele kirefu cha pili barani Afrika kikiwa mita 5,199 na hii ni hazina nyingine ya Afrika Mashariki.