Mapigano mapya yazuka siku chache kabla ya Tshisekedi na Kagame kutiliana saini mkataba wa amani
Katika taarifa yake kuhusu mapigano hayo, Jeshi la Ulinzi la nchini DRC (FARDC), limeituhumu Rwanda kwa kushirikiana na kikundi cha waasi wa M23 kwa kuratibu mfululizo wa mashambulizi katika maeneo ya Kaziba, Katogota na Lubarika.