Rais wa Marekani Donald Trump Alhamisi hii atawakutanisha viongozi wa Rwanda na DRC mjini Washington, ambapo watatia saini makubaliano ya amani, ikiwa ni miezi kadhaa kupita tangu makubaliano ya awali yaliyosimamiwa na Washington kushindwa kuzuia machafuko mwashariki mwa Congo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mwezi Juni rais Trump alikutana na mawaziri wa mambo ya nje toka nchi hizo mbili ambapo walitia Saini makubaliano ya awali, yaliyompa nguvu Trump kuelekea kile amesema kumalizika kwa vita vya mashariki mwa Congo.
Licha ya makubalino ya mwezi Juni, mapigano mashariki mwa Congo hayajakoma, huku kila upande ukimtuhumu mwingine kutoheshimu mkataba wa kusitisha mapigano, huku hadi sasa ikiwa haifahamiki ikiwa utiaji Saini wa viongozi wa wajuu kutasaidia kumaliza mzozo kati yao.

Rwanda inayowasaidia waasi wa M23, ina mamia ya wanajeshi wake mashariki mwa Congo, jambo ambalo ndilo limekuwa na mvutano katika majadiliano yanayoendelea, Kinshasa ikitaka Kigali iache kuwasaidia waasi hao na kuondoa wanajeshi kwenye ardhi yake.
Mwishoni mwa juma lililopita rais Felix Tshisekedi kupitia msemaji wake Tina Salama, alithibitisha kuwa atahudhuria shughuli hiyo saw ana mwenzake Paul Kagame, ambaye katika hotuba ya Alhamisi iliyopita alionesha matumaini madogo hata kama atatia Saini makubaliano na Kinshasa.

Haya yakiendelea, rais Kagame amemteua Dr Usta Kayitesi kama Waziri wa masuala ya ukanda na mambo yan je, akichukua nafasi ya aliyewahi kuwa mkuu wa majeshi Jenerali James Kabarebe, ambaye ameteuliwa kuwa mshauri wa masuala ya ulinzi na usalama kwenye ofisi ya rais.