Uteuzi huu umefanyika kabla ya kikao cha saba cha Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA7, kitakachofanyika Nairobi, kenya

Amani, ambaye ana wafuasi zaidi ya milioni moja mitandaoni, ni miongoni mwa mwanawake mashuhuri wa muziki wa kufokafoka au rap barani katika Ukanda wa Afrika Mashariki na wanahabari wa vyombo vya habari.

Amefanikiwa kushinda tuzo nyingi, ikiwa ni pamoja na Tuzo ya Miji ya Muziki inayotambua na kusherehekea matumizi bora ya muziki kuendeleza maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kimazingira, na kitamaduni katika miji na maeneo duniani pamoja na Tuzo ya Orange nchini Tanzania.

Mazingira yamekuwa mlinzi wetu

Wakati tunakua, tulishuhudia asili kama mlinzi mkuu ikitoa maji, chakula, kivuli, na maana. Pia tumeona kuwa inakuwa hatarini zaidi kutokana na mabadiliko ya tabianchi na matumizi yasiyo endelevu, yakisababisha mafuriko na ukame. Kwa kujiunga na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, nataka kuhamasisha mashabiki wangu kuwa sehemu ya kizazi kilichoazimia kurejesha mazingira. Sasa siyo tena kutilia maanani hasara ya asili lazima tuirejeshe. Sisi ni Kizazi cha Ukarabati,” amesema  Amani.

Amani anakuwa mchechemuzi wa kwanza wa UNEP kwa urejeshaji wa mifumo ya ikolojia. Katika wadhifa huu, atafanya kazi kuongeza uelewa na kuhamasisha vijana kukomesha, kuzuia kuendelea, na kurekebisha uharibifu wa mazingira.

UNEP imesema wakati wa katikati ya muongo wa Umoja wa Mataifa wa Urejeshaji wa Mazingira, sauti yake iko tayari kuimarisha juhudi za kurejesha mazingira katika maeneo ya asili yaliyoharibika kuanzia baharini hadi milimani na kutoka miji hadi savana, nyasi, na misitu.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, Inger Andersen amesema Frida anaimba, anazungumza, na anafanya kazi kwa ajili ya mazingira yenye afya, kwa hivyo nina furaha kumkaribisha katika familia ya UNEP, Kazi yake inaonesha shauku isiyo na kikomo kwa urejeshaji, ambapo kujali watu na asili kunakwenda sambamba, na kumfanya kuwa mfano wa kuigwa kwa vijana kote Afrika na zaidi.”

Mchango wa Frida Amani

Mchango wa Amani katika masuala ya kijamii na kimazingira umejumuishwa katika utengenezaji na maonesho mengi ya muziki wake.

Hii inajumuisha nyimbo kama Kisiki Hai, ambao ni urejeshaji wa asili unaosimamiwa na wakulima, tamasha kwa ajili ya mazingira, kampeni ya Mote Mama Gizani kwa afya ya wanawake wajawazito, pamoja na jukumu lake kama Balozi wa Haki kwa wakfu wa lead au Lead Foundation.

Frida Amani pia ameanzisha wakfu  wake  Amani Foundation  ambao unaunga mkono miradi kama tamasha la mazingira lililofanyika Tanzania mwanzoni mwa mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *