
Umoja huo unasema karibu watu laki tatu wameachwa bila makao katika miezi ya hivi karibuni katika eneo hilo.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia Wakimbizi UNHCR Xavier Creach, amesema machafuko yamesababisha karibu watu laki moja kulikimbia eneo la kaskazini mwa Msumbiji katika kipindi cha wiki mbili zilizopita pekee.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva,Creach amesema huenda ikawa idadi hiyo iko chini kwani hao ni wale walioandikishwa na UNHCR tu ila kuna visa vingi zaidi vya watu ambao hawakujiandikisha ila walikimbia.
Amesema shirika hilo la Umoja wa Mataifa limeshuhudia ongezeko la mashambulizi katika vijiji na machafuko hayo kufikia hata maeneo yaliyokuwa salama.