
Haya yanafanyika wakati idadi ya vifo vilivyotokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi ya wiki iliyopita ikipindukia 1,300.
Ripoti zinaarifu kuwa zaidi ya watu 900 wengine hawajulikani walipo.Kulingana na mamlaka mafuriko na maporomoko hayo yaliwauwa watu zaidi ya 700 Indonesia, zaidi ya 400 Sri lanka na karibu 200 nchini Thailand na 3 nchini Malaysia.
Lakini Rais wa Sri Lanka, Anura Kumara Dissanayake amesemani mapema mno kufahamu idadi kamili ya watu walioaga dunia nchini humo.
Nchi ya Indonesia ambayo iliathirika pakubwa na mkasa huo, waokoaji wanapitia kipindi kigumu kuvifikia vijiji katika kisiwa cha Sumatra ambako barabara zimesombwa na maji na madaraja kuvunjika.